Tuesday, December 1, 2015

MHE. BALOZI WILSON M. MASILINGI, BALOZI WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGMZO NA MKURUGENZI MTENDAJI WA BENKI YA DUNIA, KANDA YA AFRIKA, BW. LOUIS RENE PETER LAROSE. TAREHE 30.11.2015 KATIKA OFISI YA BENKI YA DUNIA

Mhe. Wilson M. Masilingi, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani, akifuatana na Bw. Paul Mwafongo alihudhuria mkutano na Bw. Louis Rene Peter Larose, Mkurugenzi Mtendaji, Benki ya Dunia, Kundi la Nchi za Afrika. Wengine waliohudhuria ni pamoja na Bw. Andrew Ndaamunhu Bvumbe, Mkurugenzi Mtendaji Mbadala Benki ya Dunia, Kanda ya Afrika, na Bw. WilsonToninga Banda, Mshauri, Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji.

Shabaha ya Mkutano ilikuwa ni kufuatilia mazungumzo yaliyofanyika Lima, Peru kuhusu kuimarisha ushirikiano kwa maslahi ya Afrika. Mhe. Balozi Masilingi alishukuru Benki ya Dunia kwa ushirikiano mzuri uliopo na kwa misaada na mikopo wanayotoa kuunga mkono juhudi za kujenga uchumi na kufanikisha mipango ya maendeleo kwa manufaa ya Watanzania wote. Aidha aliwahakikishia ushirikiano muda wote atakapokuwa katika kutekeleza wajibu wake wa kazi kwa maslahi ya Taifa. Mkurugenzi Mtendaji Benki ya Dunia, Kanda la Afrika, Bw. Louis Larose, alieleza kwa upande wake kuridhirishwa kwake na ushirikiano uliopo baina ya Tanzania na Benki ya Dunia. Aidha Bw. Larose aliipongeza Tanzania kwa kufanikisha Uchaguzi Mkuu uliofanyika tarehe 25 Oktoba , 2015 kwamba ulikuwa huru na wa haki. Pia, alimpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. John P. Magufuli kwa ushindi na kwa juhudi zake katika kuangalia udhibiti wa ukusanyaji wa mapato ya serikali na kuziba mianya ya uvujaji wa mapatao ili zipatikane fedha kwa ajili ya kusukuma maendeleo ya Watanzania.

Mkurugenzi Mtendaji aliahidi kwamba Benki ya Dunia iko tayari kutoa msaada wowote wa haraka utakaohitajika na kuombwa na Serikali ya Tanzania ili kufanikisha mpango wa kukusanya mapato ya ndani kwa ajili ya kutekeleza program za maendeleo na huduma za serikali.

Bw. Larose, alimdokeza Mhe. Balozi kwamba Benki ya Dunia itaandaa siku maalumu mjini Washington, D.C. kwa ajili ya kuitangaza Tanzania na vivutio vyake nchini Marekani na kuomba kwamba Benki ya Dunia itamwalika Mhe. Balozi kuzindua siku hiyo. Akijibu hoja hiyo Mhe. Balozi alikubali mwaliko huo.


Mhe. Wilson M. Masilingi, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani, (Katikati) akiwa na Bw. Louis Rene Peter Larose, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia, Kanda ya Afrika (mkono wa kushoto wa Balozi) Wengine Bw. Paul Mwafongo, Mwambata Uchumi wa Ubalozi (wa kwanza kushoto), Bw. Andrew Ndaamunhu, Mkurugenzi Mtendaji Mbadala, Kanda ya Afrika (wapili kushoto) na Bw. Wilson Toninga Banda, Mshauri, Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji (wa kwanza kulia)


Mhe. Balozi Wilson M. Masilingi (kushoto) katika picha ya pamoja na Bw. Louis Rene Peter Larose, Mkurugenzi Mtendaji, Kanda ya Afrika (kushoto), Ofisi za Benki ya Dunia


Mhe. Balozi Wilson M. Masilingi (kushoto) katika mazungumzo ofisini kwa mwenyeji wake Bw. Louis Rene Peter Larose.

1 comment:

  1. Do you need personal loan?
    Loan for your home improvements,
    Mortgage loan,
    Debt consolidation loan,
    Commercial loan,
    Education loan,
    Car loan,
    Loan for assets.
    financialserviceoffer876@gmail.com WhatsApp +918929509036

    ReplyDelete