Wednesday, December 30, 2015

Mikutano ya Mhe. Balozi Wilson M. Masilingi Oakland, California Dec. 19, 2015

Katika ziara ya Mhe. Balozi Wilson M. Masilingi ya Oakland, California alikutana na wafanyabiashara katika sekta ya utalii wanaopeleka watalii Tanzania katika kampuni zao. Mhe. Balozi aliongea nao kujua changamoto wanazopata katika kupeleka watalii Tanzania, kwaajili ya kutengeneza mkakati wa kuongeza idadi ya watalii wanaoenda huko. Baada ya maongezi yao, Mhe. Balozi aliwaahidi kufuatilia mazungmzo yao na kuendelea kushirikiana katika mpango wa kuongeza idadi ya watalii. Baada ya mkutano huo Mhe. Balozi alitembelea ofisi ya Hon. Consul Bw. Ahmed Issa. 

Mhe. Balozi Wilson M. Masilingi pamoja na Hon. Consul Bw. Ahmed Issa na Wafanyabiashara wa Utalii na Wadau mbalimbali wa Elimu 


Bw. Bill Roberson wa INCA, Perry Roberson wa Blue Odyssey Tours, Brenda Ross wa Sister City na Bw. Alan Feldstein wa Infinite Safari Adventures


Honurary Consul wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, California Bw. Ahmed Issa

Tuesday, December 29, 2015

End of the Year Message of H.E Ambassador Wilson Masilingi to the Tanzanians living in the United States. 
H.E Ambassador Wilson Masilingi delivered his end of year message which called Tanzanians living in the United States of America to strengthen their cooperation and continue to be good Ambassadors of the United Republic of Tanzania to the United States of America. He also highlighted various activities that, the government of the United Republic of Tanzania through the Embassy in the United States is implementing in realization of the Economic Diplomacy. Ambassador’s message reiterated all Tanzanians in the United to engage in various economic and social initiatives so as to contribute to the country socio-economic development. He further assured the Tanzania Diaspora of the Embassy cooperation and readiness to collaborate in any initiative of interest to the people of Tanzania and the Country in General.

Thursday, December 3, 2015

MHE. BALOZI WILSON MASILINGI AKUTANA NA MHE. BALOZI HUNAINAH ALMUGHEIRY WA OMAN WASHINGTON DCMhe. Wilson Masilingi, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani akikaribishwa ofisini kwa Mhe. Balozi Hunaina Almugheiry, Balozi wa Oman nchini Marekani.

Mheshimiwa Wilson Masilingi, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani alimtembelea Mhe. Hunainah AlMugheiry, Balozi wa Oman nchini Marekani, ofisini kwake Washington DC leo Alhamisi Desemba 3,2015. Katika mazungumzo Mhe. Balozi Masilingi aliambatana na Bw. Suleiman Ahmed Saleh, Afisa wa Ubalozi wa Tanzania Washington DC.

Mazungumzo kati ya Mhe. Balozi Masilingi na Mhe. Mugheiry yalilenga katika kuimarisha mahusiano kati ya nchi hizo mbili zenye mahusiano ya kidugu. Mhe. Balozi Mugheiry alifurahishwa na kuonana na Mhe. Masilingi na kubainisha kwamba Oman na Tanzania zina mahusiano ya kidamu na hivyo nchi hizo hazina budi kudumisha mahusiano hayo ya kihistoria. Mhe. Mugheiry alimweleza Balozi Masilingi kwamba amefarijika uchaguzi wa Tanzania ulikwisha salama na Tanzania kumpata mrithi wa Rais mpya Mhe. John Pombe Magufuli kufuatia kumaliza muda wake Rais aliyepita Mhe. Jakaya Kikwete.Aliongeza kwa kusema kwamba Oman na Tanzania zimekuwa na mashirikiano ya kiuchumi,kibiashara na kielimu na anaamini kwamba ujenzi wa bandari ya Bagamoyo na fursa za masomo ya juu zinazotolewa na Serikali ya Oman kwa wanafunzi wa Tanzania Bara na Visiwani ni vielelezo vya mahusiano hayo.

Kwa upande wake Mhe. Balozi Masilingi alifarijika sana kumsikia Mhe. Balozi Hunainah wa Oman akimwambia kwamba alizaliwa Dar-es-Salaam, Tanzania, na familia yake ina mizizi visiwani Zanzibar pia. Alimshukuru Balozi Hunainah kwa kumkaribisha ofisini kwake na kufahamiana naye na kuahidi kufanya naye kazi kwa karibu katika kuendeleza mahusiano baina ya nchi zao zenye mahusiano ya asili.

Mhe. Wilson Masilingi katika picha ya kumbukumbu na Mhe. Hunainah Almugheiry

TANGAZO


UBALOZI WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, 
WASHINGTON, D.C.
 
TANGAZO

Mhe. Balozi Wilson M. Masilingi anawakaribisha Watanzania wote na Wamarekani wenye asili ya Kitanzania kwenye mkutano mfupi wa kufahamiana utakaofanyika tarehe 12 Desemba, 2015.

Mkutano huo utafanyika katika ukumbi wa Tabeer uliopo 1401 University Boulevard, Hyattsville Maryland 20783, kuanzia saa tisa hadi saa kumi na moja jioni (3:00pm – 5:00pm).

Wote mnakaribishwa, na tafadhali zingatieni muda.

Tuesday, December 1, 2015

MHE. BALOZI WILSON M. MASILINGI AKUTANA NA BI. CATHY BYRNE, MKURUGENZI MWANDAMIZI WA MASUALA YA AFRIKA, IKULU YA MAREKANI (WHITE HOUSE) TAREHE 30 NOVEMBA 2015

Mhe. Balozi Masilingi alitembelea ofisi ya Bi. Cathy Byrne, Mkurugenzi Mwandamizi wa masuala ya Afrika katika Ikulu ya Marekani (White House). Wakati wa mazungmzo yao, Bi. Cathy Byrne alimueleza Mhe. Balozi Masilingi kuwa Serikali ya Marekani inaridhishwa na mahusiano mazuri yaliyopo baina yake na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Marekani. Aidha alieleza kuwa Serikali ya Marekani inaridhishwa na hatua mbalimbali zinachukuliwa na serikali ya Tanzania, katika kuwaletea wananchi wake maendeleo.

Mhe. Balozi Masilingi amemhakikishia mwenyeji wake kuwa ataendeleza mashirikiano mazuri sana yaliyopo kati ya serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Marekani kwa njia ya diplomasia ya uchumi yenye lengo la kuhamasisha biashara na uwekezaji nchini Tanzania.


Mhe. Balozi Wilson M. Masilingi akiagana na Bi. Cathy Byrne mara baada ya kumaliza mazungmzo yao.

MHE. BALOZI WILSON M. MASILINGI, BALOZI WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGMZO NA MKURUGENZI MTENDAJI WA BENKI YA DUNIA, KANDA YA AFRIKA, BW. LOUIS RENE PETER LAROSE. TAREHE 30.11.2015 KATIKA OFISI YA BENKI YA DUNIA

Mhe. Wilson M. Masilingi, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani, akifuatana na Bw. Paul Mwafongo alihudhuria mkutano na Bw. Louis Rene Peter Larose, Mkurugenzi Mtendaji, Benki ya Dunia, Kundi la Nchi za Afrika. Wengine waliohudhuria ni pamoja na Bw. Andrew Ndaamunhu Bvumbe, Mkurugenzi Mtendaji Mbadala Benki ya Dunia, Kanda ya Afrika, na Bw. WilsonToninga Banda, Mshauri, Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji.

Shabaha ya Mkutano ilikuwa ni kufuatilia mazungumzo yaliyofanyika Lima, Peru kuhusu kuimarisha ushirikiano kwa maslahi ya Afrika. Mhe. Balozi Masilingi alishukuru Benki ya Dunia kwa ushirikiano mzuri uliopo na kwa misaada na mikopo wanayotoa kuunga mkono juhudi za kujenga uchumi na kufanikisha mipango ya maendeleo kwa manufaa ya Watanzania wote. Aidha aliwahakikishia ushirikiano muda wote atakapokuwa katika kutekeleza wajibu wake wa kazi kwa maslahi ya Taifa. Mkurugenzi Mtendaji Benki ya Dunia, Kanda la Afrika, Bw. Louis Larose, alieleza kwa upande wake kuridhirishwa kwake na ushirikiano uliopo baina ya Tanzania na Benki ya Dunia. Aidha Bw. Larose aliipongeza Tanzania kwa kufanikisha Uchaguzi Mkuu uliofanyika tarehe 25 Oktoba , 2015 kwamba ulikuwa huru na wa haki. Pia, alimpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. John P. Magufuli kwa ushindi na kwa juhudi zake katika kuangalia udhibiti wa ukusanyaji wa mapato ya serikali na kuziba mianya ya uvujaji wa mapatao ili zipatikane fedha kwa ajili ya kusukuma maendeleo ya Watanzania.

Mkurugenzi Mtendaji aliahidi kwamba Benki ya Dunia iko tayari kutoa msaada wowote wa haraka utakaohitajika na kuombwa na Serikali ya Tanzania ili kufanikisha mpango wa kukusanya mapato ya ndani kwa ajili ya kutekeleza program za maendeleo na huduma za serikali.

Bw. Larose, alimdokeza Mhe. Balozi kwamba Benki ya Dunia itaandaa siku maalumu mjini Washington, D.C. kwa ajili ya kuitangaza Tanzania na vivutio vyake nchini Marekani na kuomba kwamba Benki ya Dunia itamwalika Mhe. Balozi kuzindua siku hiyo. Akijibu hoja hiyo Mhe. Balozi alikubali mwaliko huo.


Mhe. Wilson M. Masilingi, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani, (Katikati) akiwa na Bw. Louis Rene Peter Larose, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia, Kanda ya Afrika (mkono wa kushoto wa Balozi) Wengine Bw. Paul Mwafongo, Mwambata Uchumi wa Ubalozi (wa kwanza kushoto), Bw. Andrew Ndaamunhu, Mkurugenzi Mtendaji Mbadala, Kanda ya Afrika (wapili kushoto) na Bw. Wilson Toninga Banda, Mshauri, Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji (wa kwanza kulia)


Mhe. Balozi Wilson M. Masilingi (kushoto) katika picha ya pamoja na Bw. Louis Rene Peter Larose, Mkurugenzi Mtendaji, Kanda ya Afrika (kushoto), Ofisi za Benki ya Dunia


Mhe. Balozi Wilson M. Masilingi (kushoto) katika mazungumzo ofisini kwa mwenyeji wake Bw. Louis Rene Peter Larose.