Wednesday, December 30, 2015

Mikutano ya Mhe. Balozi Wilson M. Masilingi Oakland, California Dec. 19, 2015

Katika ziara ya Mhe. Balozi Wilson M. Masilingi ya Oakland, California alikutana na wafanyabiashara katika sekta ya utalii wanaopeleka watalii Tanzania katika kampuni zao. Mhe. Balozi aliongea nao kujua changamoto wanazopata katika kupeleka watalii Tanzania, kwaajili ya kutengeneza mkakati wa kuongeza idadi ya watalii wanaoenda huko. Baada ya maongezi yao, Mhe. Balozi aliwaahidi kufuatilia mazungmzo yao na kuendelea kushirikiana katika mpango wa kuongeza idadi ya watalii. Baada ya mkutano huo Mhe. Balozi alitembelea ofisi ya Hon. Consul Bw. Ahmed Issa. 

Mhe. Balozi Wilson M. Masilingi pamoja na Hon. Consul Bw. Ahmed Issa na Wafanyabiashara wa Utalii na Wadau mbalimbali wa Elimu 


Bw. Bill Roberson wa INCA, Perry Roberson wa Blue Odyssey Tours, Brenda Ross wa Sister City na Bw. Alan Feldstein wa Infinite Safari Adventures


Honurary Consul wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, California Bw. Ahmed Issa


Mhe. Balozi Wilson M. Masilingi akiandika katika kitabu cha wageni.


Mhe. Balozi akiwa na Bw. Ahmed Issa na mke wake.


Mhe. Balozi akionyeshwa magari ya kampuni ya Bw. Ahmed Issa.

IMG_7727.JPG

1 comment: