Mhe.
Liberata Mulamula, Balozi wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania nchini
Marekani amemkaribisha Mhe. Ammon Mutembwa, Balozi mpya wa Jamhuri ya
Zimbabwe Ubalozini Tanzania House, Washington DC, Marekani, Jumatano
Novemba 26, 2014. Katika mazungumzo yake na Balozi Mutembwa, Mhe. Balozi
Mulamula alimweleza Balozi huyo kwamba ajisikie kwamba yuko nyumbani.
Mhe. Mulamula aliendelea kwa kusema kwamba Tanzania na Zimbabwe zina
mahusiano ya kihistoria na kwa msingi huo ni vyema kutafsiri kwa vitendo
mahusiano hayo kwa kujenga mashirikano zaidi baina yao. Mhe. Mulamula
alifurahishwa na ziara hiyo ya Balozi Mutembwa Ubalozini na kuahidi
kwamba kupitia kwa Jumuia ya Ushirikiano wa Nchini za Kusini mwa Afrika
(SADC), Tanzania na Zimbabwe zina fursa ya kutosha kuziwakilisha nchi
zao nchini Marekani kwa manufaa ya Serikali na wananchi wao.
Kwa
upande wake, Mhe. Balozi Mutembwa alimshukuru Mhe. Balozi Mulamula kwa
kumkaribisha Ubalozini na kwamba kwa vile ndio kwanza ameripoti katika
kituo chake kipya cha kazi atashukuru sana kupata mwongozo wake na
ushauri kutoka kwake ili aweze kutekeleza majukumu yake ya kiuwakilishi
nchini Marekani kwa ufanisi. Balozi Mutembwa alisema pia kwamba moja ya
jukumu lake kubwa ni kuhakikisha vikwazo ilivyoekewa nchi yake na
Marekani vinaondolewa kupitia mazungumzo na kujenga maelewano mazuri baina ya nchi yake na Marekani.
Mhe.Balozi Mulamula na Mhe. Balozi Mutembwa katika picha ya kumbukumbu baada ya kusaini kitabu cha wageni.
Mhe. Balozi Liberata Mulamula(Katikati) akiwa katika mazungumzo na mgeni wake Mhe.Balozi Ammon Mutembwa (Wa pili kushoto) huku Maofisa wao Bw. Suleiman Saleh (Wa kwanza kulia) na Bw. Whatmore Goora (Wa kwanza kushoto) wakifuatilia.
Do you need personal loan?
ReplyDeleteLoan for your home improvements,
Mortgage loan,
Debt consolidation loan,
Commercial loan,
Education loan,
Car loan,
Loan for assets.
financialserviceoffer876@gmail.com WhatsApp +918929509036