Honourable
Deputy Speaker,
Various local and
international media reported yesterday that members of the delegation of the
President of China, who visited our country 18 months ago, engaged in buying
ivory in the country. The source of the allegation is apparently a report by an
American Non-Governmental Organisation known as Environmental Investigation
Agency (EIA). The report further accused
our country and its leaders of passivity and doing nothing to stem illegal
ivory trade.
Honourable
Deputy Speaker,
Allow me to inform the
Tanzanian public and the international community through your august House,
that the claims by the American NGO that the historic visit to Tanzania by the
Chinese President, who chose our country for his first trip abroad after
assuming office, was associated with
illegal ivory trade, have no iota of truth. Similarly, accusations the
Government of Tanzania pays no attention to illegal ivory trade and takes no
action against culprits of the crime, are baseless. The EIA report has been
cooked up with the aim of tainting the good reputation of our country and that
of our friends, the People’s Republic of China. It is a patched up report,
whose release has been timed to serve an agenda well known to us.
Honourable
Deputy Speaker,
Before delving into why
I hold that this report is fabricated, allow me to outline to your august House
the following six undisputed facts:
1) Firstly, it is true
that the biggest ivory market is in China. Those engaged in illegal ivory trade
look for market in China;
2) It is also
undisputed that most of the ivory peddled in the black market originates from
African countries, including Tanzania;
3) The illegal ivory
trade involves criminals and criminal networks masterminded by individuals of
different nationalities, including Chinese and Tanzanians;
4) The Government of
Tanzania and that of China are not engaged in illegal ivory trade and have no
link with criminal networks of the illicit trade.
5) Cognizant of the
gravity of the effects of illegal ivory trade, our two governments have been
working very closely in tackling the criminal networks of the illicit business.
Government agencies in our two countries have been collaborating and exchanging
information, which led to the arrest of culprits. Furthermore, during the
recent visit to China by our President, our two governments signed an agreement
under which China would provide equipment for an operation to fight poaching
and illegal harvesting of forest resources in Tanzania (China Aided Equipment
for Forest Resources and Wildlife Conservation). Another agreement was signed
for China to provide modern equipment for cargo surveillance at the port.
6) Tanzania and China participated
fully at the London Confrrence on Illegal Wildlife Trade, which was held in
February, 2014. One of the major achievements of that meeting was the signing
of an agreement to fight illegal ivory mtrade by China, Botswana and Tanzania. This
was the first time for China to sign such agreement, which attests to the
commitment by the government of President Xi Jinping to rout illegal ivory
trade. Before the London conference, the Chinese government burnt in public a
consignment of illegal ivory seized in the country.
Honourable
Deputy Speaker,
Having said that, allow
me now to explain why I submitted that the reports by the NGO EIA are
fabricated.
Honourable
Deputy Speaker,
This was not the first
time for the New York Times to publish such report. A similar
report was published last year. The
source of the allegations mentioned in the report is a person met on the street
and interviewed. The person is not an employee at the port or airport. He is
just a commoner as seen in the video clip of the interview.
Apart from the false
allegations made by suspect source, the EIA report also mentioned the
interception of a container at the port with illegal ivory. It is true that
state agencies intercepted the container with contraband. What was not
publicized is that the seizure was made possible by close cooperation of
Tanzanian and Chinese intelligence agencies. It was intelligence information
from China which facilitated the operation. Disappointingly, however, reports
in social media claimed that the intercepted container was being loaded onto a
Chinese naval ship, which was not true.
It must also be
mentioned that President Xi’s visit to Tanzania lasted for 24 hours and his
programme started immediately on arrival at 15.00 hours ending at 22.00 hours
with a state banquet on the first day. The second day’s programme started in
the morning with the inauguration of Mwalimu Julius Nyerere International
Convention Centre, after which President Xi and his delegation had meetings
with Zanzibar President, Dr. Ali Mohamed Shein and retired President Benjamin
William Mkapa. Thereafter, President Xi and his delegation proceeded to the
Chinese cemetery at Majohe from where they drove to the airport and flew off.
The question is, what time did the alleged shopping carried out by President
Xi’s delegation take place?
And why should the
allegations of President Xi and his delegation buying illegal ivory arise
today? Why now after the visit by our President to China? Why should the report
be published after the national address by our President in which he detailed
the success of his visit to China?
Honourable
Deputy Speaker,
Everybody can guess the
answers. The peddlers of such reports do not wish our country well. They do not
wish our Chinese friends well. They are jealous of China’s achievements. It is
amazing that they hate them while they depend so much on them. They would wish
to monopolize Chinese trade, Chinese financing and Chinese investments. It is
taboo for us Africans to access those opportunities. We must not accept such
nonsense. We are an independent country, nobody will choose friends for us and
we shall not inherit anybody’s enemies. We will enhance our brotherly
partnership with China and we shall not be deterred by malicious fabrications
from any quarter.
Let me also reassure your
august House, Honourable Deputy Speaker, that our government will not relent in
the fight against illegal ivory trade. The days of perpetrators of the evil
business are numbered.
Thank you for your kind
attention.
ISSUED
BY: THE MINISTRY OF FOREIGN AFFAIRS AND INTERNATIONAL COOPERATION, DAR ES
SALAAM
7TH
NOVEMBER, 2014
______________________________
TAARIFA KWA
VYOMBO VYA HABARI
Wizara
ya Matnbo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa inawasilisha kwenye Vyombo vya
Habari taarifa kuhusu Kauli ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Kimataifa, Mhe. Bernad K.Membe (Mb.) kama alivyoitoa Bungeni leo tarehe 07
Novemba, 2014 Mjini Dodoma kuhusu shutuma dhidi ya Serikali za China na Tanzania
kujihusisha na biashara haramu ya Pembe za Ndovu.Taarifa hiyo llitolewa kwa
mujibu wa Kanuni ya 49 (1) ya Kanuni za Kudumu za Bunge Toleo la 2013. Taarifa
hiyo inasomeka kama liuatavyo:-
KAULI YA
WAZIRI WA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA
KIMATAIFA KUHUSU SHUTUMA DHIDI YA
SERIKALI ZA CHINA NA TANZANIA
KUJIHUSISHA NA BIASHARA HARAMU YA PEMBE ZA NDOVU INAYOTOLEWA KWA MUJIBU WA
KANUNI YA 49 (1) YA KANUNI ZA KUDUMU ZA BUNGE TOLEO LA 2013
Mheshimiwa
Naibu Spika,
Siku ya Jana Vyombo vya Habari
mbalimbali vya Ndani na Nje ya Nchi vilitoa habari kwamba ujumbe wa Rais wa
China uliokuja nchmi Miezi 18 iliyopita ulijihusisha na ununuzi wa pembe za
ndovu nchmi. Chanzo cha habari hizo ni taarifa ya taasisi isiyo ya kiserikali
ya nchini Marekani ijulikanayo kama Environmental Investigation Agency (EIA).
Habari hiyo imekwenda mbali zaidi kuituhumu nchi yetu na viongozi
wake kutojali, wala
ushughulikia tatizo la biashara haramu ya pembe za ndovu.
Mheshimiwa
Naibu Spika,
Ninapenda
kupitia Bunge lako tukufu kuutaarifu umma wa Watanzaniana dunia
kwa ujumla kwamba madai yaliyotolewa na NGO hiyo ya Marekani ya kuihusisha ziara ya
kihistoria ya Rais wa China kutembelea Tanzania kama nchi
ya kwanza toka aingie madarakani na biashara haramu ya pembe za ndovu hayana
ukweli wowote. Vilevile, madai ya kwamba Serikali ya Tanzania haijali na wala
haichukui hatua dhidi ya wanaojishughulisha na biashara haramu ya pembe za
ndovu sio kweli.
Taarifa za
taasisi hii ya EIA (Environmental Investigation Agency) ni za kupikwa na
kuungwa ungwa ili kuchafua heshima ya nchi yetu, pamoja na kuchafua heshima ya
rafiki zetu wa Taifa la China. Ni taarifa iliyoandaliwa na kutolewa wakati huu
ili kukidhi ajenda mahususi ambayo tunaifahamu fika.
Mheshimiwa
Naibu Spika,
Kabla sijaelezea kwanini ninasema taarifa hii sio ya
kweli ningependa kwanza kulielezea Bunge lako tukufu mambo sita yafuatayo
ambayo hayana ubishi:
1)
Moja, ni kweli soko kubwa la pembe za ndovu lipo China. Wanaofanya
biashara haramu ya pembe za ndovu hutafuta soko huko;
2)
Ni ukweli usiopingika kwamba pembe za ndovu nyingi zinazouzwa kwenye
masoko haramu zinatokea katika nchi za Afrika, Tanzania ikiwa ni miongoni mwa
nchi zinapotoka pembe hizo;
3) Biashara hiyo haramu inahusisha
wahalifu/ na mitandao ya wahalifu ambao wana uraia wa nchi mbalimbali zikiwemo
China na Tanzania:
4) Serikali ya Tanzania na Serikali
ya China hazifanyi biashara
haramu ya pembe
za ndovu na wala hazihusiki na mitandao haramu.
5)
Kwa kutambua ukubwa wa Tatizo la biashara hiyo haramu, Serikali zetu
mbili zimekuwa na ushirikiano wa karibu kabisa katika kukabiliana na mitandao
inayofanya biashara hiyo haramu. Vyombo vya dola vya nchi zetu mbili
vimeshirikiana kwa karibu na kupashana habari kila wakati zilizowezesha
kuwakamata wahusika wa biashara hiyo. Isitoshe wakati wa ziara iliyomalizika
hivi majuzi Serikali zetu mbili zilisaini mkataba wa kutupatia vifaa vya
kusaidia operesheni ya kupambana na ujangili wa wanyamapori - (China Aided
Equipment for Forest Resources and Wildlife Conservation). Vilevile kwenye
ziara hiyo tulisaini Mkataba wa kutupatia mitambo ya kisasa ya kufanya ukaguzi
wa mizigo bandarini- ambayo itasaidia kubaini mizigo inayosafirishwa.
6) Tanzania na China zilishiriki
kikamilifu kwenye Mkutano wa Kimataifa wa Kudhibiti Biashara Haramu ya Pembe za
ndovu (London Confrrence on Illegal Wildlife Trade) uliofanyika mwezi Februari
2014. Moja ya mafanikio makubwa ya mkutano huo ni kwa nchi za China, Botswana
na Tanzania kusaini mkataba wa kupambana na biashara hiyo haramu. Hii ilikuwa
ni mara ya kwanza kwa China kusaini Mkataba wa aina hiyo, jambo
lililodhihirisha umakini wa Serikali ya Rais Xi Jinping kushughulikia tatizo la
biashara haramu. Vilevile kabla ya mkutano huo wa London, Serikali ya China
ilichoma moto hadharani shehena ya meno ya tembo haramu yaliyokuwa
yakishikiliwa nchini humo.
Mheshimiwa
Naibu Spika,
Baada ya kusema
hayo, naomba sasa naomba nitoe sababu kwanini ninasema habari za NGO ya EIA ni
za uongo;
Mheshimiwa
Naibu Spika,
Taarifa kama hii
iliyotoka kwenye New York Times sio mara ya kwanza kutolewa. Taarifa ya aina
hii iliwahi kutolewa mwaka jana. Na mtoa taarifa ambaye ametajwa kuwa chanzo
cha habari ni mtu mmoja ambaye walimkuta barabarani na kuanza kumuuliza maswali
wanasema. Mtu huyo sio mtumishi wa bandari wala uwanja wa ndege. Ni mpita njia
tu wa mtaani. Hata video ya mahojiano ya Aljazeera inaonyesha hivyo. Ukiachilia
mbali uwongo uliotolewa na bwana huyo, taasisi ya EIA imeongelea tukio la
kontena lililokamatwa Bandarini likiwa na pembe za ndovu.
Ni kweli kabisa
kwamba kontena la pembe lilikamatwa bandarini na vyombo vya dola. Jambo moja
ambalo watu wengi hawalijui ni kwamba mafanikio ya operesheni ile yalitokana na
ushirikiano wa vyombo vya usalama vya Tanzania na China. Taarifa za
kiinteligensia juu ya operation hiyo kwakweli zilitoka China na kuwasilishwa
taarifa hiyo kwenye Serikali ya Tanzania na ndipo operesheni ile ilipofanikiwa.
Lakini habari zilizotoka kwenye mitandao zilisema kwamba Kontena limekamatwa
likipelekwa kwenye meli ya kijeshi ya China...jambo ambalo sio kweli hata
kidogo. (Msisitizo) Huwezi Serikali ya China ukaleta taarifa ya intelijensia
Tanzania ya kuonyesha kuna kontena linakuja China, halafu wakati huohuo,
Serikali ya China imetayarisha meli yake ya kijeshi kubeba hiyo kontena. Ni
uongo ambao hauwezi kukubalika.
Mbali na hayo, ziara ya Rais Xi
Jinping nchini ilikuwa ya masaa 24 tu, na programu yake ilianza mara tu
alipowasili nchini kuanzia saa 9 alasiri hadi saa 4 usiku kwenye dhifa ya
taifa. Siku ya pili ratiba ilianza asubuhi kwa uzinduzi wa Ukumbi wa Mikutano
ya Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere. Baada ya hapo Rais Xi na ujumbe wake
walikuwa na mikutano na Rais wa Zanzibar Mhe Dk. Ali Mohamed Shein na Rais
Mstaafu wa awamu ya tatu Mhe. Benjamin William Mkapa. Baada ya hapo Rais Xi na
ujumbe wake walienda kwenye makaburi ya Wachina kule Majohe na kisha wakaondoka
kwenda uwanja wa ndege. Sasa hizo shopping zinazoelezewa kufanywa na ujumbe wa
Rais Xi Jin Ping zilifanyika saa ngapi? Zilifanyika usiku wa manane?
Jambo muhimu la
kujiuliza hapa, ni je hiyo taarifa ya Rais Xi na ujumbe wake kubeba pembe za
ndovu iweje itoke leo? Kwanini wakati huu baada ya ziara ya Rais wetu nchini
China? Kwanini
itoke baada ya Mhe Rais Kikwete kuhutubia kuhusu mafanikio ya ziara yake nchini
China? Jibu ni moja tu. Wivu.
Wasambazaji wa
taarifa hizi hawaitakii mema kabisa nchi yetu. Hawawatakii mema marafiki zetu
wa China.
•
Wakubwa hawa hawataki tujengewe reli ya TAZARA na reli ya kati kwa
viwango vya kisasa kabisa.
•
Wakubwa hawa hawataki tujengewe bandari ya Bagamoyo, bandari ya kisasa
ambayo italeta makontena mengi na meli nyingi katika nchi yetu.
•
Hawataki tupatiwe mikopo nafuu kwa ajili ya maendeleo ya nchi yetu.
• Na wala hawataki tujenge vyuo
vya ufundi nchini, achia mbali kutaka kupata scholarships nyingi kutoka China
kwa ajili ya Watanzania haswa katika upande wa gesi na mafuta.
Wanaweka wivu,
hawataki na sisi tuendelee kama walivyoendelea wenzetu. Inashangaza kuona,
wanawachukia lakini huku wakiwategemea Wachina hao hao. Wao wangependa peke yao
wafanye biashara na China, wakachukue mikopo China, wavutie uwekezaji kutoka
China, lakini tukifanya sisi Watanzania au Waafrika inakuwa nongwa. Tusikubali
upuuzi wa aina hii. Sisi ni taifa huru, hatuwezi kuchaguliwa marafiki wala
hatutarithishwa maadui. Tutaendeleza ushirikiano wetu wa kidugu na China na
kamwe hatutorudi nyuma kutokana na maneno ya uwongo na uzushi.
Aidha, ninapenda
kulihakikishia Bunge lako Tukufu Mheshimiwa Naibu Spika kwamba Serikali yetu
haitorudi nyuma. Tutaendeleza mapambano dhidi ya biashara haramu ya pembe za
ndovu. Na wale wote wanaoshughulika na biashara hizo, siku zao zimefikia
mwisho.
Ahsanteni kwa
kunisikiliza.