Thursday, November 20, 2014

MHE. MOHAMED CHANDE OTHMAN, JAJI MKUU WA TANZANIA ATEMBELEA UBALOZI WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, WASHINGTON DC 19/11/2014

Mhe. Mohamed Chande Othman, Jaji Mkuu wa  Tanzania ametembelea Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania uliopo Washington DC na kufanya mazungumzo na wafanyakazi wa Ubalozi huo Ubalozini hapo Tanzania House. Katika mazungumzo yake hayo, Mhe. Chande aliwaeleza watumishi wa Ubalozi namna mihimili mitatu ya dola inavyofanya kazi pamoja na mipaka yake. Alibainisha kwamba Tanzania inajivunia mahusiano mazuri yaliyopo baina ya mihimili hiyo ambayo kutokana na misingi thabiti imekuwa ikifanya kazi katika mazingira mazuri yanayojikita katika kulisukuma taifa la Tanzania mbele. Mhe. Chande alisema pia Tanzania imo katika juhudi kubwa za kuhakikisha wananchi wake wanapata huduma za kimahakama katika kila ngazi ili kukidhi mahitaji yaliyopo sasa katika mikoa mbali mbali.

Aliongeza kwamba jambo la msingi  kwa sasa ni kuongeza ufanisi katika shughuli za kimahakama na hili linahitaji zaidi rasilimali fedha ili vyombo vyote viweze kutekeleza majukumu yake kwa wakati muafaka.


Mhe. Mohamed Chande, Jaji Mkuu wa Tanzania akisaini kitabu cha wageni katika Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Washington DC, Marekani.

Mhe. Mohamed Chande Othman, Jaji Mkuu wa Tanzania (Wa Tatu Kushoto)katika picha ya pamoja na Maofisa wa Ubalozi wa Tanzania Washington DC na watumishi wengine wakati wa ziara yake Ubalozini. Wa nne Kushoto, ni Mhe. Prof. Ibarahim Juma, Jaji wa Mahakama ya Rufaa na wa Pili kulia ni Mhe. Aloysius Mujulizi, Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania.



1 comment:

  1. Do you need personal loan?
    Loan for your home improvements,
    Mortgage loan,
    Debt consolidation loan,
    Commercial loan,
    Education loan,
    Car loan,
    Loan for assets.
    financialserviceoffer876@gmail.com WhatsApp +918929509036

    ReplyDelete