Mhe.
Wilson M. Masilingi, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini
Marekani, akifuatana na Bw. Paul Mwafongo alihudhuria mkutano na Bw.
Louis Rene Peter Larose, Mkurugenzi Mtendaji, Benki ya Dunia, Kundi la
Nchi za Afrika. Wengine waliohudhuria ni pamoja na Bw. Andrew Ndaamunhu
Bvumbe, Mkurugenzi Mtendaji Mbadala Benki ya Dunia, Kanda ya Afrika, na
Bw. WilsonToninga Banda, Mshauri, Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji.
Shabaha
ya Mkutano ilikuwa ni kufuatilia mazungumzo yaliyofanyika Lima, Peru
kuhusu kuimarisha ushirikiano kwa maslahi ya Afrika. Mhe. Balozi
Masilingi alishukuru Benki ya Dunia kwa ushirikiano mzuri uliopo na kwa
misaada na mikopo wanayotoa kuunga mkono juhudi za kujenga uchumi na
kufanikisha mipango ya maendeleo kwa manufaa ya Watanzania wote. Aidha
aliwahakikishia ushirikiano muda wote atakapokuwa katika kutekeleza
wajibu wake wa kazi kwa maslahi ya Taifa. Mkurugenzi Mtendaji Benki ya
Dunia, Kanda la Afrika, Bw. Louis Larose, alieleza kwa upande wake
kuridhirishwa kwake na ushirikiano uliopo baina ya Tanzania na Benki ya
Dunia. Aidha Bw. Larose aliipongeza Tanzania kwa kufanikisha Uchaguzi
Mkuu uliofanyika tarehe 25 Oktoba , 2015 kwamba ulikuwa huru na wa haki.
Pia, alimpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. John P.
Magufuli kwa ushindi na kwa juhudi zake katika kuangalia udhibiti wa
ukusanyaji wa mapato ya serikali na kuziba mianya ya uvujaji wa mapatao
ili zipatikane fedha kwa ajili ya kusukuma maendeleo ya Watanzania.
Mkurugenzi
Mtendaji aliahidi kwamba Benki ya Dunia iko tayari kutoa msaada wowote
wa haraka utakaohitajika na kuombwa na Serikali ya Tanzania ili
kufanikisha mpango wa kukusanya mapato ya ndani kwa ajili ya kutekeleza
program za maendeleo na huduma za serikali.
Bw. Larose,
alimdokeza Mhe. Balozi kwamba Benki ya Dunia itaandaa siku maalumu mjini
Washington, D.C. kwa ajili ya kuitangaza Tanzania na vivutio vyake
nchini Marekani na kuomba kwamba Benki ya Dunia itamwalika Mhe. Balozi
kuzindua siku hiyo. Akijibu hoja hiyo Mhe. Balozi alikubali mwaliko huo.
Mhe.
Wilson M. Masilingi, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini
Marekani, (Katikati) akiwa na Bw. Louis Rene Peter Larose, Mkurugenzi
Mtendaji wa Benki ya Dunia, Kanda ya Afrika (mkono wa kushoto wa Balozi)
Wengine Bw. Paul Mwafongo, Mwambata Uchumi wa Ubalozi (wa kwanza
kushoto), Bw. Andrew Ndaamunhu, Mkurugenzi Mtendaji Mbadala, Kanda ya
Afrika (wapili kushoto) na Bw. Wilson Toninga Banda, Mshauri, Ofisi ya
Mkurugenzi Mtendaji (wa kwanza kulia)
Mhe.
Balozi Wilson M. Masilingi (kushoto) katika picha ya pamoja na Bw.
Louis Rene Peter Larose, Mkurugenzi Mtendaji, Kanda ya Afrika (kushoto),
Ofisi za Benki ya Dunia
Mhe. Balozi Wilson M. Masilingi (kushoto) katika mazungumzo ofisini kwa mwenyeji wake Bw. Louis Rene Peter Larose.